1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rutto: Nina furaha kuwa mtazamaji kwani sitolaumiwa kwa kashfa za wizi wa mabilioni ya shillingi

21 Agosti 2020

https://p.dw.com/p/3hIBh

Katika kile kinachoonekana kuwa ishara ya wazi kabisa kuwa mambo yanaendelea kutokoka katika serikali ya Jubilee nchini Kenya, Naibu wa Rais William Ruto amejitokeza kwa mara nyingine na kusema kuwa ana furaha kwamba kwa sasa yeye ni mtazamaji tu katika serikali kwa sababu hatolaumiwa kwa kashfa za wizi wa mabilioni ya shillingi zinazoikumba serikali ya Rais Uhuru Kenyatta. Katika kupata ufafanuzi kujua iwapo kauli ya Ruto inadhihirisha kuvunjika rasmi kwa ndoa ya kisiasa kati ya Ruto na Uhuru, Bruce Amani amezungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa Alutalala Mukhwana akiwa Nairobi.