Ruto: Mpango wa kutuma askari wa Kenya, Haiti unaendelea
30 Januari 2024Kikosi hicho cha kimataifa kinanuiwa kwenda kukabiliana na vurugu za magenge ya wahumi na wabeba silaha ambayo yameuteteresha usalama wa Haiti ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya karibu watu 5,000.
Hatma ya ujumbe huo iliingia mashakani baada ya mahakama ya mji wa Nairobi kutoa uamuzi kuwa upelekeaji askari wa Kenya nchini Haitiitakuwa kinyume na katiba isipokuwa kama kutakuwa na makubaliano na serikali ya nchi hiyo.
Soma pia:Serikali ya Kenya yaapa kupinga uamuzi wa mahakama dhidi ya kupeleka maafisa wa polisi nchini Haiti
Kwenye mahojiano na shirika la habari la Reuters, rais Ruto amesema mipango tayari itaelendelea ya kutumia pendekezo hilo la mahakama la kuwepo mkataba wa nchi mbili kuwezesha ujumbe huo wa kulinda amani kutumwa nchini Haiti.
Amesema tayari Haiti ilituma maombi rasmi kwa serikali ya Kenya na mipango inafanyika kutuma polisi nchini humo.