SiasaAsia
Ruto ataka uwekezaji zaidi wa China barani Afrika
19 Oktoba 2023Matangazo
Ruto ameyasema hayo katika Kongamano la Miundombinu ya Usafirishaji la China, ambalo lilimalizika siku ya Jumatano (Oktoba 18) na kuongeza kwamba uboreshaji wa miundombinu ungetafsiriwa kuwa "kiwango cha juu cha muunganisho unaohakikisha mabadiliko halisi," kufungua demokrasia ya ushirikishwaji na kutoa fursa zisizo na kikomo kwa Afrika.
Soma zaidi: Ruto asema mabadiliko ya tabianchi yanatafuna maendeleo ya Afrika
Kiongozi huyo wa Kenya alikuwa anatafuta kiasi cha dola bilioni 1 kufadhili miradi iliyokwama, na tayari amepata kiasi cha dola bilioni 4.6 katika mikataba ya uwekezaji kutoka kwa makampuni binafsi ya China.