Rushdie apokea Tuzo ya Amani ya maonesho ya vitabu Ujerumani
23 Oktoba 2023Mwandishi vitabu raia wa Uingereza mzaliwa wa India Salman Rushdie ametunukiwa tuzo ya amani ya maonyesho ya vitabu ya Ujerumani mjini Frankfurtjana Jumapili katika hafla iliyogubikwa na mizozo ya sasa duniani. Akizungumza katika kanisa la kihistoia mjini Frankfurt, Rushdie, mwenye umri wa miaka 76, alisema ameshukuru sana kwa tuzo hii kubwa lakini amani kwa sasa ni kama ndoto.
Rushdie aidha alisema tunaishi wakati ambao hakufikiri angeishi kuuona katika maisha yake ambapo uhuru, hususan wa kujieleza ambao bila huo ulimwengu wa vitabu haungekuwepo, unashambuliwa kote na kauli za misimamo mikali, kiimla, kizalendo na zisizojali.
Tuzo ya amani ya maonyesho ya vitabu ya Ujerumani inatolewa pamoja na kitita cha euro 25,000 na inachukuliwa kuwa tuzo muhimu zaidi nchini Ujerumani.