1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rusessabagina awasili Qatar

28 Machi 2023

Paul Rusesabagina, shujaa aliyeangaziwa katika filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 amewasili nchini Qatar baada ya kuachiliwa huru na serikali ya Kigali.

https://p.dw.com/p/4PM0d
Ruanda Paul Rusesabagina
Picha: Cyril Ndegeya/Xinhua/IMAGO

Paul Rusesabagina, shujaa aliyeangaziwa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, ya Hotel Rwanda, amewasili nchini Qatar baada ya kuachiliwa huru kutoka jela nchini Rwanda wiki iliyopita.

Hayo yameelezwa  leo na chanzo chenye taarifa kuhusu suala hilo.

Soma zaidi: Rusesabagina aachiwa huru

Aliachiwa huru Ijumaa wiki iliyopita baada ya kifungo chake kufutwa kufuatia miezi kadhaa ya mazungumzo kati ya Marekani na Rwanda. 

Imeelezwa kwamba Russesabagina, mwenye umri wa miaka 68, aliwasili jana Jumatatu mjini Doha.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani atarejea nchini Marekani akitokea Doha.