Rudisha: mchezo wa riadha unachafuliwa
4 Machi 2016Zaidi ya wanariadha 40 wa Kikenya wamegunduliwa kutumia virutubisho vilivyopigwa marufuku katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hali iliyolilazimu Shirika la Kimataifa la Kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini – WADA kuweka tarehe ya mwisho ya Aprili 5 kwa Kenya kuidhinisha sheria ya kulishughulikia tatizo hilo.
Ikiwa hilo halitafanyika, basi Kenya huenda ikafungiwa kushiriki katika Michezo ya Olimpiki mjini Rio mwezi Agosti "Ni vigumu sana kwa shirika la kupambana na dawa zilizopigwa marufuku michezoni kudhibiti hali kwa sababu kuna maelfu na maelfu ya Wakenya wanaopewa mafunzo na ni wachache tu walio kwenye orodha ya WADA. Wanariadha chipukizi ni tatizo kubwa kwa sababu hawajulikani, hakuna anayewahamu na kisha wanapokwenda mashindanoni kwa mara ya kwanza, wananaswa, lakini ni vizuri , kwa sababu inaonyesha kuwa mashirika ya kupambana na dawa hizo yanafanya kazi yao.
Maafisa wakuu watatu wa riadha Kenya wamesimamishwa kazi na Chama cha Kimataifa cha mashirikisho ya Riadha – IAAF, wakisubiri matokeo ya uchunguzi wa kamati yake ya maadili kuhusiana na tuhuma za kuficha matokeo ya vipimo vya dawa za kuongeza nguvu misuli.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu