1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Formula one: Rosberg ashinda Mexico

2 Novemba 2015

Nico Rosberg alipata ushindi wake wa kwanza katika kipindi cha miezi minne baada ya kumpiku mwenzake wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton katika mashindano ya magari ya Formula One ya Mexican Grand Prix

https://p.dw.com/p/1GyTH
Formel 1 GP Mexiko Rosberg Siegerehrung
Picha: Getty Images/M. Thompson

Mjerumani huyo alitawala mbio hizo kutoka mwanzo hadi mwisho huku akifwatwa kwa karibu na bingwa mpya wa dunia Hamilton. Valtteri Bottas wa timu ya Williams alimaliza katika nafasi ya tatu.

Ushindi huo wa Rosberg, ambao ndio wake wa nne msimu huu, umemrejesha katika nambari mbili kwenye msimamo wa ubingwa wa ubingwa wa dunia akiwa nyuma ya Sebastian Vettel wa timu ya Ferrari ambaye hakuweza kumaliza mbio hizo baada ya kupata ajali.

Hayo yalikuwa mashindano ya Grand Prix ya kwanza kuandaliwa Mexico katika kipindi cha miaka 20

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu