ROME:Wajerumani watiririka Rome kumuona Papa mpya
23 Aprili 2005Matangazo
Hadi Wajerumani 100,000 wanatazamiwa kumiminika mjini Rome siku ya jumapili kushuhudia,Kadinali wa zamani Joseph Ratzinger,alie mzaliwa wa Ujerumani,akisoma misa ya uzinduzi kama Baba Mtakatifu Benedikt wa 16.Kansela Gerhard Schroeder na Rais Horst Koehler wa Ujerumani pia watakwenda Rome kuungana na viongozi wengine mashuhuri wa kimataifa.Zaidi ya viongozi 200 kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanatazamiwa kuhudhuria misa ya siku ya Jumapili.Inakadiriwa kuwa siku hiyo hadi watu nusu milioni watakusanyika kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro.Siku ya Ijumaa Baba Mtakatifu,alikuwa na mkutano wake wa kwanza wa hadhra katika Vatikan pamoja na makadinali wa kanisa la Katoliki