1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME:Solana na wapatanishi wa nyuklia wa Iran wakutana

24 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7D1

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana na wapatanishi wa maswala ya nyuklia wa Iran wanaendelea na mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.

Bwana Solana amesema kwamba mazungumzo hayo yanaelekea vizuri wakati alipokutana na wazairi wa mambo ya nje ya Italia Massimo D’Alema mapema leo pia anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Italia Romano Prodi baadae leo.

Waziri mkuu wa Italia kisha atakutana na mpatanishi mpya wa maswala ya nyuklia wa Iran Saeed Jalili pamoja na mtangulizi wake Ali Larijani.

Italia sio mwanachama katika kundi linalojadili maswala ya nyuklia ya Iran lakini ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa taifa hilo.

Italia pia sio mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa mwaka huu.