1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME:Mtuhumiwa wa mipango ya kuripua mabomu London kurejeshwa Uingereza kutoka Italia.

18 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEk1

Mahakama moja ya Italia imeidhinisha kupelekwa nchini Uingereza,kwa mtu wanayemshikilia anayetuhumiwa kuhusika na mipango ulioshindwa wa kuushambulia mji wa London kwa mabomu mwezi uliopita.Mtu huyo Osman Hussain ambaye pia anafahamika kwa jina la Hamdi Isaac,alitiwa mbaroni katika mji mkuu wa Italia,Rome siku chache baada ya kushindwa kwa mpango huo terehe 21 Julai.

Akitoa tamko la idhini hiyo hakimu wa mahakama hiyo alisema watamkabidhi Husaain kwa serikali ya Uingereza katika kipindi cha siku 35 zijazo.

Mawakili wa Huseein wamepewa siku kumi kukata rufaa kupinga amri hiyo ya kupelekwa Uingereza kwa mteja wao.