1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME:mjumbe mpya wa Iran bado ashindikizwa na Larijani mjini Rome

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DT

Mjumbe mpya wa Iran juu ya suala la nyuklia la nchi hiyo leo anaingia katika jukwaa la kimataifa mjini Rome kwa mara ya kwanza, ambapo atashiriki kwenye mazungumzo yatakayozipa fursa nchi za magharibi kubaini iwapo Iran imezidi kuwa na msimamo mkali juu ya mpango wake wa nyuklia.

Mjumbe huyo mpya bwana Saeed Jalili anatazamiwa kukutana na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana.

Bwana Jalili ataongozana na mjumbe wa hapo awali bwana Ali Larijani alietangaza kujiuzulu mwishoni mwa wiki iliyopita.