ROME:Bunge laridhia fedha zaidi kwa jeshi la Italia nchini Afghanistan
28 Machi 2007Matangazo
ROMA
Waziri Mkuu wa Italia, Romano Prodi amefanikiwa kupata kura za kutosha bungeni zinazomruhusu kupata fedha za ziada kwa ajili ya majeshi ya nchi hiyo huko Afghanistan.
Mwezi uliyopita suala hilo liliibua mzozo serikalini, wakati Waziri Mkuu huyo wa Italia alipopigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Massimo D´ Alema amepongeza hatua hiyo akisema kuwa kushindwa kupitishwa kwa muswaada huo wa kuongeza fedha kwa kikosi cha askari elfu mbili wa Italia katika jeshi la NATO ingekuwa aibu.