ROME. Waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi ajiuzulu.
21 Aprili 2005Waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi amejiuzulu kutoka wadhifa wake. Rais Carlo Azeglio Ciampi amemtaka Berlusconi ashikilie wadhifa huo, huku akishauriana na washiriki wake wa kisiasa katika juhudi za kuunda serikali mpya.
Berlusconi amewaambia waandishi habari mjini Rome kwamba anataraji mazungumzo hayo yatakamilika kufikia mwishoni mwa juma hili. Iwapo hatafanikiwa kufanya hivyo, rais Ciampi huenda alivunje bunge na kuitisha uchaguzi mapema.
Serikali ya Berlusconi ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa tangu Ijumaa iliyopita, wakati chama kimoja cha kisiasa kilipojiondoa kutoka kwa serikali hiyo ya muungano. Chama kingine nacho kimetishia kujiondoa kutoka muungano huo, kikitaka mabadiliko muhimu yafanywe kufuatia kushindwa vibaya kwa muungano huo katika uchaguzi wa mikoa.