1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Waziri mkuu Berlusconi anatarajiwa kujiuzulu.

20 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLC

Waziri mkuu wa Italia Bwana Silvio Berlusconi anatarajiwa kujiuzulu ili kuunda serikali mpya ya mseto. Bwana Berlusconi akilihutubia bunge leo amesema atajiuzulu na kujaribu kuunda serikali mpya ili kuunusuru muungano katika serikali yake ambao unalegalega.

Muungano huo umeingia katika hali ya wasi wasi zaidi kutokana na kitisho kutoka katika chama cha pili ambacho kinataka kujitoa. Chama cha National Alliance kimesema kuwa mawaziri wake watano huenda wakajiondoa katika baraza la mawaziri la Bwana Berlusconi baada ya kubadilisha uamuzi wake jana wa kujiuzulu. Badala yake Bwana Berlusconi ameitisha kura ya kuwa na imani na utawala wake. Hii inakuja baada ya kuondoka wiki iliyopita kwa mawaziri wanne wa chama kingine kinachounda muungano wa serikali cha Union of Christian Democrats.

Viongozi wake wamedai mabadiliko ya sera baada ya kundi hilo kuanguka katika uchaguzi wa mikoa.