1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME. Waumini wa kikatoliki waruhusiwa kulitazama kaburi la Yohana Paulo wa pili.

13 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNc

Waumini wa dini ya kikatoliki na raia waliruhusiwa kuanzia leo kulitazama kaburi la marehemu Yohana Paulo wa pili, aliyezikwa katika chumba cha siri chini ya kanisa la Mtakatifu Petro. Mamia ya waumini walijumuika katika misafara kulitazama kaburi hilo. Eneo hilo lilikuwa limefungwa tangu Ijumaa iliyopita na hakuna aliyeruhusiwa kuingia. Mabaki ya Petro Mtakatifu, mwanafunzi wa Yesu aliyelianzisha kanisa la Kristo yako mahala hapo. Makadinali wa kanisa katoliki wanatarajiwa kukutana juma lijalo kumchagua papa mpya atakayeliongoza kanisa hilo.