ROME: Watalii wa Kitaliana wameachiliwa huru
14 Oktoba 2006Matangazo
Watalii 2 wa Kitaliana wameachiliwa huru baada ya kutekwa nyara mwezi wa Agosti nchini Niger.Wizara ya mambo ya kigeni ya Italia imenukuliwa kusema kuwa Watalii hao waliachiliwa huru katika ardhi ya Libya na imetoa shukrani kwa maafisa wa Kilibya kwa mchango wao wa kusaidia kupata uhuru wa mateka hao.Wataliana hao wawili walikuwa katika kundi la watalii lililotekwa nyara na majambazi wenye silaha tarehe 21 Agosti kusini-mashariki mwa Niger karibu na mpaka wa Chad. Watalii wengine waliachiliwa huru hapo awali bila ya kudhuriwa.