1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Wakimbizi wakamatwa katika boti.

26 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEql

Maafisa wa Italia wamewapeleka kiasi cha wakimbizi 360 katika kisiwa cha Lampedusa kusini mwa nchi hiyo.

Boti iliyokuwa imewachukua kiasi wakimbizi 130 iligunduliwa kiasi maili 50 kutoka kisiwani hapo, wakati chombo kingine kilichokuwa na watu 224 kilikamatwa karibu na pwani ya kisiwa hicho cha Lampedusa.

Watu hao wanaotaka ukimbizi wamepelekwa katika kituo ambapo wamezuiliwa.

Maafisa nchini Italia wamesema zaidi ya wakimbizi 800 wamewasili katika kisiwa hicho cha Lampedusa na Sicily katika muda wa wiki moja.