ROME: Wakimbizi 13 wamefariki Bahari ya Kati
30 Julai 2006Matangazo
Ripoti za jeshi la wanamaji la Italia,zasema watu 13 waliojaribu kufika Ulaya kwa njia isiyo halali wamefariki katika boti kwa sababu ya njaa na kiu baada ya kuelea kwa muda wa siku 20 katika Bahari ya Kati.Wengine 14 waliokolewa na manowari ya jeshi la wanamaji la Italia,umbali wa kama kilomita 230 kutoka kusini ya kisiwa cha Lampedusa.Watu wengine 150 waliokimbilia Ulaya kwa njia isiyo halali,walifanikiwa kutua Sicily na Lampedusa kwa usalama katika boti nne.