1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Wahamiaji wasio halali 650 wagutukiwa

26 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCg4

Walinzi wa mwambao nchini Italia wameigutukia mashua ya mita 30 yenye wahamiaji wasio halali takriban 650 karibu na kisiwa cha Sicily.

Hiyo ni idadi kubwa ya Waafrika kuwahi kushuhudiwa wakijaribu kujipenyeza Ulaya wote wakiwa kwenye mashua moja. Wahamiaji hao wanaosema kuwa ni raia wa Misri wamepelekwa kwenye mji wa bandari wa Sicily wa Licata.

Takriban mashua zote zenye kuwasili huko Sicily au Lampedusa ambavyo ni vituo mashuhuri kwa wahamiaji wasio halali huwa hazibebi zaidi ya watu 200.

Jumamosi iliopita wahamiaji 102 wamepotea baharini kwenye mwambao wa Senegal katika bahari ya Atlantiki baada ya mashua yao kupinduka.

Ni watu tu 25 walinusurika.