1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Ulinzi waimarishwa Vatican kutokana na shambulizi la kigaidi mjini London.

9 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvw

Kutokana na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya mji wa London , makao makuu ya kiongozi wa kanisa Katoliki ya Vatican mjini Rome yametangaza hatua za usalama kwa ajili ya Pope pamoja na makaazi yake.

Kwa mujibu wa ripoti katika gazeti la, La Reppublica, Pope Benedikt hatasafiri tena katika gari la wazi katika mji wa Rome.

Badala yake atasafiri katika gari ya kawaida likiwa na vioo visivyopenya risasi.

Hatua nyingine za kiusalama katika Vatican ni pamoja na vifaa zaidi vya kutambua vitu vya chuma kuzunguka uwanja wa St. Peter, kamera za video katika kanisa la St. Peter Basilika na kupigwa marufuku ndege zote kupita juu ya eneo la Vatican.