1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME. Uhusiano kati ya Italy na Marekani waingia doa

27 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIn

Matokeo ya uchunguzi wa kwanza wa Marekani juu ya mauaji ya Afisa wa upelelezi yanayodaiwa kufanywa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq yamewaghadhabisha watu wa Italy.

Nicola Calipari aliuwawa mapema mwezi uliopita kwa kupigwa risasi alipokuwa akimsindikiza nyumbani Giuliana Sygrena, muandishi habari wa Italy aliyekuwa ameshikwa mateka nchini Iraq.

Kifo cha afisa huyo kimezusha hasira na ghadhabu nchini Italy na kusababisha kuharibika kwa uhusiano kati yake na Marekani.

Kwa mujibu wa Afisa mmoja Marekani ambaye hakutaja jina lake ripoti ya uchunguzi huo inatarajiwa kueleza kwamba gari alilokuwa akiendesha Marehemu Carlipari halikufuata ishara ya kupunguza kasi katika kituo cha ukaguzi wa magari madai ambayo yamepingwa vikali na Italy.