1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Serikali ya Itali yaungwa mkono katika mswada wa mageuzi ya sheria

21 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEsN

Serikali ya waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi, imeshinda kura ya imani juu ya mswada unaopendekeza mabadiliko ya sheria. Berlusconi amesema mswada huo uliozozaniwa ni hatua muhimu katika kuleta mageuzi kwenye vyombo vya sheria nchini humo.

Kipengele muhimu cha mswada huo kinapendekeza mahakimu na waongoza mashtaka wapigwe marufuku kuwa wanachama wa vyama vya kisiasa au vyama vya wafanyakazi. Wapinzani lakini wanasema mswada huo unauingilia uhuru wa mahakama.