1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Prodi kuchukuwa hatua kali dhidi ya vurugu za soka

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVI

Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi ameahidi kuchukuwa hatua kali kupambana na vurugu katika soka.

Prodi amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali haiko tena tayari kuhatarisha maisha ya polisi wake.Prodi alikuwa akizungunza katika muda usiozidi masaa 24 baada ya kuuwawa kwa afisa polisi katika ghasia zilizohusu pambano la soka la ligi kuu nchini Italia kati ya clabu za jimbo la Sicily za Catania Calcio na US Palermo.Hicho ni kifo cha pili kuhusiana na soka kutokea katika kipindi cha wiki moja nchini Italia.

Chama cha Soka nchini Italia kimefuta michezo yote ya ligi na ile ya kimataifa kwa muda usiojulikana.

Mkutano wa dharura kati ya mawaziri wa mambo ya ndani na michezo unatazamiwa kufanyika hapo Jumatatu.