1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Pope Benedikt nae atoa wito kwa mataifa yenye utajiri wa viwanda kujitahidi kuuondoa umasikini katika bara la Afrika.

4 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CExY

Kiongozi wa kanisa katoliki Pope Benedikt wa 16 amejiunga na sauti za kimataifa zinazotaka viongozi wa kundi la mataifa yenye utajiri mkubwa wa viwanda duniani G8, kuchukua hatua za kufuta umasikini katika bara la Afrika.

Hii inakuja baada ya wanamuzi maarufu duniani kufanya matamasha kadha yaliyojulikana kama , Live 8 , katika kutoa mbinyo kwa viongozi hao wa G8 kuchukua hatua zaidi kupambana na umasikini katika bara la Afrika.

Matamasha hayo ya muziki yamepangwa kufanyika siku chache tu kabla ya mkutano wa mataifa hayo ya G8 nchini Scotland.

Suala la Afrika na hali ya hewa duniani ni agenda za juu kabisa katika mkutano huo.