1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Papa yuko katika hali njema

26 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFax

Makao makuu ya kanisa katoliki Vatican imesema Papa John Paul wa Pili anapumzika akiwa katika hali njema kufuatia operesheni ya roho katika hospitali ya Rome.

Papa alirudishwa tena hospitali hapo Alhamisi kutokana na matatizo ya kupumuwa.Msemaji wa Vatican amesema Papa mwenye umri wa miaka 84 alikuwa akipumuwa mweyewe bila ya msaada wa mashine.

Wakristo wa madhehebu ya Katoliki duniani kote wamekuwa wakimuombea Munga Papa huyo apate nafuu huku madaktari wakielezea wasi wasi wao juu ya mzigo kwa afya ya Papa mwenye umri mkubwa kwa kuzingatia kuumwa kwake sana mara kadhaa kulikotishia maisha yake huko nyuma,athari za ugonjwa wa kutetemeka aliokuwa nao pamoja na tabia ya kukaidi ushauri wa kimatibabu.