ROME: Papa mpya akutana na waandishi habari
23 Aprili 2005Matangazo
Baba Mtakatifu mpya Benedikt wa 16,kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake,amekutana na waandishi habari kutoka sehemu mbali mbali za dunia.Katika hotuba fupi aliyotoa kwa lugha nne tofauti amesema,angependa kuendeleza uhusiano na vyombo vya habari kama ilivyokuwa na mtangulizi wake,marehemu Yohanna Paulo wa Pili.Kwa wakati huo huo amevikumbusha vyombo vya habari wajibu wake wakati wa kuripoti masuala yanayohusika na imani.Kwa hivi sasa mji wa Rome unajitayarisha kwa sherehe ya kutawazwa Papa mpya siku ya jumapili.