1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Papa kutoendesha Sala ya Bikira Maria

27 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFan

Papa John Paul wa Pili leo hatoendesha Sala ya jadi ya Bikira Maria mjini Rome kwa mara ya kwanza kabisa tokea awe papa miaka 26 iliopita.

Taarifa ya makao makuu ya kanisa katoliki Vatikan imesema msaidizi wake ataendesha sala hiyo na kuubariki umati katika uwanja wa St.Peter lakini Papa atashiriki kwa ishara akiwa katika chumba chake cha hospitali.Papa amelazwa hospitali tokea Alhamisi kutokana na matatizo ya kupumuwa ambapo amekuwa hawezi kutowa sauti kwa muda sasa kutokana na operesheni ya roho iliokuwa na lengo la kumpatia nafuu kwa matatizo hayo ya kupumuwa.

Bado hakuna taarifa yoyote ile kwa muda gani ataendelea kubakia hospitalini.