1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Papa John Paul wa Pili azikwa, maelfu wahudhuria mazishi yake.

9 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOz

Karibu kila sehemu duniani, watu wa imani mbali mbali walihudhuria katika makanisa na maeneo ya wazi wakifanya sala ya kumuaga Papa Yohana Paulo wa pili, jana . Viongozi zaidi ya 200 wa kisiasa na kidini pamoja na maelfu kadha ya watu walijazana katika uwanja wa st. Peter katika eneo la Vatican kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo wa kanisa Katoliki.

Mkusanyiko mmojawapo mkubwa pia ulikuwa katika mji wa kusini mwa Poland wa Krakow, ambako kiasi cha watu nusu milioni walihudhuria.. Kiongozi huyo wa kidini aliwahi kuwa askofu wa mji huo kabla ya kuchaguliwa kuwa Pope mwaka 1978. Mamilioni zaidi ya watu duniani waliona mazishi hayo kupitia televisheni.