ROME: Papa amewaalika wajumbe wa kiislamu
23 Septemba 2006Matangazo
Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amewaalika mabalozi wa nchi za kiislamu katika Vatikan na hata viongozi wa kidini wa Kiislamu kuhudhuria mkutano utakaofanywa siku ya Jumatatu katika nyumba yake ya mapumziko Castel Gandolfo nje ya Rome.Afisa wa ngazi ya juu katika Vatikan amesema,mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia kuwaeleza Waislamu waliyokasirishwa na hotuba iliyotolewa na Papa nchini Ujerumani wiki iliyopita,kuwa wamemuelewa visivyo.Iran na Uturuki zimesema huenda zikapeleka wajumbe wao kwenye mkutano huo, siku ya Jumatatu.