1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Papa akasimu Misa ya Mtende ya Jumapili

20 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFV7

Papa John Paul wa Pili amejitokeza kwa muda mfupi kwenye dirisha la nyumba yake makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatikani kuwabariki maelfu ya mahujaji wanaohudhuria misa ya Jumapili ya Mtende.

Hii ni mara ya kwanza tokea ashike wadhifa wa Upapa miaka 26 iliopita Papa John Paul hakusimamia Misa hiyo ya Mtende ya Jumapili ambayo inaadhimisha kuingia kwa Yesu Kristo mjini Jerusalem kabla ya hatimae Kusulubiwa msalabani na Ufufuo wake.

Papa John Paul bado anaendelea kupata nafuu kutokana na operesheni ya koo na bado haijulikani lini Papa huyo mwenye umri wa miaka 84 ataweza kuanza kazi zake za kawaida.