ROME: Njaa duniani ni hatima inayoweza kuzuilika
16 Oktoba 2007Matangazo
Rais wa Ujerumani,Horst Köhler ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana kupiga vita njaa,kote duniani.Amesema,lazima ziwepo siasa aminifu za maendeleo,chini ya msingi wa ushirikiano.Rais Köhler alikuwa akihotubia Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Chakula na Kilimo-FAO mjini Rom kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani.Rais Köhler akasisitiza,njaa ni hatima inayoweza kuzuilika.
Kwa mujibu wa FAO,kote duniani,watu milioni 854 wana njaa-milioni 820 wapo katika nchi zinazoendelea.Wakati huo huo,Papa Benedikt XVI amesema,njaa ni ukiukaji wa hadhi ya binadamu.