ROME: Niger yakabiliwa na balaa la njaa kubwa
27 Julai 2005Matangazo
Niger inakabiliwa na ukosefu mkubwa sana wa chakula,lakini hiyo ni moja tu kati ya nchi chungu nzima katika Afrika ya Magharibi zinazokabiliwa na njaa na mara nyingi husahauliwa na wafadhili.Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa WFP,linalotoa misaada ya chakula.Msemaji wa WFP,Chris Andean amesema,balaa za kimaumbile,mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na umasikini ni mambo yaliosambaa katika nchi hizo.Kwa mujibu wa WFP,Niger yenye watu milioni 2.5 inakabiliwa na njaa kubwa baada ya kukumbwa na ukame na nzige.Hivi sasa ndio misaada imeanza kuwasili katika sehemu zilizoathirika vibaya zaidi.