ROME : Mugabe awashutumu Bush na Blair kuwa ni mashetani wa milinia
17 Oktoba 2005Matangazo
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewashutumu Rais George W Bush wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair kuwa ni mashetani wawili wa miliniea hii.
Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya Shirika la la Chakula la Umoja wa Mataifa Mugabe amewashutumu viongozi hao wawili kuwa ni magaidi wa kimataifa kwa kuanzisha vita nchini Iraq na kwa madai ya kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi katika nchi ndogo kama ile ya kwake.
Amesema Marekani na Uingereza zimejichukulia majukumu ya kuziamulia nchi zinazoendelea na hata kuingilia kati katika masuala ya ndani ya nchi na kutaka kuleta kile wanachokiita mabadiliko ya utawala.
Mugabe ametowa shutuma hizo mwishoni mwa hotuba ya kuadhimisha miaka 60 ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kwenye makao yake makuu mjini Rome