Rome. Mugabe awashambulia Bush na Blair.
18 Oktoba 2005Matangazo
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewashambulia sana rais wa Marekani George W. Bush na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, akiwaeleza kuwa ni watu wasiomjua Mungu na magaidi wa kimataifa.
Mugabe , akizungumza katika sherehe za miaka 60 za shirika la chakula la umoja wa mataifa mjini Rome, amewafananisha viongozi hao wawili na Hitler na Mussolini, akisema kuwa wameanzisha ushirikiano wa kikafiri na kuishambulia Iraq bila makosa.
Mugabe pia amezishutumu Marekani na Uingereza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yake.