1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Mshabiki wa mpira apigwa risasi na polisi kwa makosa

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJr

Ghasia kubwa zimezuka mjini Rom,baada ya mshabiki wa kandanda kupigwa risasi na kuuawa katika kosa lililofanywa na polisi.Kijana huyo aliekuwa na miaka 26 na mshabiki wa klabu ya mpira ya Lazio Rome,alipigwa risasi akiwa ndani ya gari yake,wakati wa ghasia za washabiki wa klabu ya Juventus Turin.Baadae vijana walishambulia kituo cha polisi karibu na uwanja wa michezo wa Olympia.Si chini ya watu 12 walijeruhiwa,miongoni mwao wakiwa askaripolisi 10.Vile vile idadi kadhaa ya watu wametiwa ndani.Mapambano na polisi yalitokea pia katika mji wa Milan na miji mingi mingine kusini mwa Italia.