1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Mpango wa chanjo kuokowa mamilioni ya watoto

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTn

Mataifa matano yanagharimia mpango wa dola bilioni moja na nusu kushajisha makampuni ya madawa kutowa chanjo za kusaidia kuzuwiya kichomi na homa ya uti wa mgongo katika matarajio ya kuokowa maisha ya watoto milioni tano na laki nne ifikapo mwaka 2030 katika nchi za kimaskini kabisa duniani.

Sehemu kubwa ya mpango huo wa kupambana na magonjwa mengine yanayosababisha maafa katika nchi hizo ambao mradi wake wa utangulizi unadhaminiwa na Italia,Canada,Norway, Urusi na Uingereza unalenga kirusi cha pneumococcal ambacho ndio sababu ya magonjwa ya kichomi na homa ya uti wa mgongo yanayouwa watu milioni moja na laki sita kila mwaka.

Rais wa Benki ya Dunia Paul Wolfowitz ni miongoni mwa wale wanaotazamiwa kuhudhuria uzinduzi wa mpango huo leo hii mjini Rome Italia.