1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Misa ya kutawazwa Baba Mtakatifu

24 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFK3

Papa Benedikt wa XVI hii leo atasheherekea misa ya kutawazwa kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Rome.Hadi Wajerumani 100,000 wanatazamiwa kumiminika Vatikan kumuona Joseph Ratzinger, mzaliwa wa Ujerumani akisheherekea misa ya kutawazwa Baba Mtakatifu.Kansela Gerhard Schroeder na Rais Horst Köhler wa Ujerumani wataungana na viongozi wengine wa kimataifa kwenye sherehe ya hii leo.Kiasi ya watu nusu milioni wanatazamiwa kutiririka kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro.Siku ya Jumamosi Papa aliwashukuru waandishi wa habari kwa kazi waliyoitekeleza kuripoti juu ya uchaguzi wa mrithi wa Baba Mtakatifu.Akizungumza na maripota na waumini kwa lugha 4 tofauti,Papa alisema vyombo vya habari viliwapa Wakatoliki kote duniani nafasi ya kushuhudia tukio hilo.