ROME: Meli yenye wakimbizi imepotea baharini
7 Agosti 2005Matangazo
Kwa mujibu wa maafisa wa mipaka ya Ulaya,juhudi za kuisaka meli iliyopotea,nje ya pwani ya kisiwa cha Kitaliana cha Lampedusa,ikiwa na wakimbizi 130,zimesitishwa kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.Meli nyingine iliokuwa na kama wakimbizi 160 kutoka Eritrea ilifanikiwa kufika kwenye kisiwa cha Linosa siku ya Jumatano.Na katika tukio jingine,maafisa wa Kigiriki waliwakamata wakimbizi 125 waliojaribu kuingia nchini kwa njia isiyo halali katika mashua ya uvuvi.Vile vile Waafrika 23 waliojaribu kukimbilia Visiwa vya Canary,walifariki baada ya mashua yao kuzama nje ya pwani,kaskazini-magharibi mwa Afrika.