ROME. Mazungumzo yaanza kuunda serikali mpya nchini Itali.
21 Aprili 2005Matangazo
Rais wa Itali, Carlo Azeglio Ciampi, ameanza mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini humo kujaribu kuunda serikali mpya. Waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi ambaye alijiuzulu kutoka wadhifa wake, anatarajiwa kuendelea kuongoza tena. Rais Ciampi amesema atafanya mashauriano rasmi na makundi yote ya kisiasa hadi kesho mchana, ambapo baadaye ataamua ikiwa Berlusconi anaungwa mkono kuchukua wadhifa wake tena.
Iwapo Berlusconi atashindwa kuunda serikali mpya, rais Ciampi huenda alivunje bunge na kuitisha uchaguzi, mwaka mmoja kabla tarehe ya uchaguzi. Berlusconi na washiriki wake wanataka kuzuia uchaguzi mkuu wa mapema kufanyika, uchaguzi ambao wadadisi wanasema watashindwa vibaya.