1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Matayarisho ya maziko ya Baba Mtakatifu

8 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPP

Waumini wa mwisho miongoni mwa mamilioni waliomiminika mjini Rome,wametoa heshima za mwisho kwa marehemu Baba Mtakatifu Yohanna Paulo wa Pili.Ingawa foleni zimefungwa,waumini kwa maelfu wanaendelea kutiririka katika mji uliosongamana sana.Polisi na wasaidizi wameufunga uwanja wa Mtakatifu Petro kwa matayarisho ya maziko yatakayofanywa hii leo na kuhudhuriwa na viongozi mia kadhaa wa kimataifa waliokwisha wasili mjini Rome.Na nchini Poland katika mji wa Krakow,takriban watu milioni moja walikusanyika kwa misa ya kumkumbuka Baba Mtakatifu aliezaliwa katika mji huo wa Poland.Hati ya wasia ya Baba Mtakatifu,iliotangazwa na Vatikan,imesema kuwa mnamo mwaka 2000 Papa alifikiria kujiuzulu kwa sababu ya afya mbaya.Siku ya jumatatu Makadinali waliokusanyika mjini Rome,wataanaza shughuli za kumchagua Papa mpya.