ROME: Matayarisho ya kumchagua Baba Mtakatifu mpya
17 Aprili 2005Matangazo
Makadinali wa kikatoliki wameanza kufanya matayarisho ya kumchagua kwa siri mrithi wa marehemu Papa Yohana Paulo wa Pili.Makadinali 115 wenye haki ya kupiga kura,watakutana katika kanisa dogo la Sistine kuanzia Jumatatu mchana na watabakia huko mpaka Papa mpya atakapochaguliwa.Makadinali hao watapiga kura hadi mara nne kila siku,mpaka upatikane uwingi unaohitajiwa.