ROME : Marekani na Italiana watafautiana juu ya mauaji ya jasusi
30 Aprili 2005Matangazo
Marekani na Italia zimesema zinatafautiana juu ya hitimisho la uchunguzi wa pamoja kwa mauaji ya mpelelezi wa Italia nchini Iraq yaliofanywa na wanajeshi wa Marekani.
Nicola Calipari aliuwawa wakati akijaribu kumkinga mateka wa Kitaliana wakati gari lao lilipokuja kushambuliwa na wanajeshi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.
Imeripotiwa kwamba wachunguzi wa Marekani wamegunduwa kuwa wanajeshi hao wa Marekani sio wa kulaumiwa.Waziri wa mambo ya nje wa Italia Giafranco Fini amesema uchunguzi tafauti wa Italia juu ya kifo cha Calipari utaendelea.
Taarifa hiyo ya pamoja ya Marekani na Italia imesema nchi hizo mbili zinaendelea kuwa marafiki licha ya tukio hilo.