ROME: Marekani lawamani kuhusu mauaji ya mpelelezi wa Italy
3 Mei 2005Matangazo
Serikali ya Italy imetoa ripoti yake inayolaumu mauaji ya mpelelezi wake wa ujasusi mjini Baghdad imetokana na ukosefu wa tajriba upande wa wanajeshi wa Marekani wanaofanya kazi wakiwa na mawazo mengi.
Wanajeshi wa Marekani walimuua Nicola Calipari alipokuwa akimsindikiza mwanahabari wa Italy aliyekuwa amewachiliwa mateka nchini Iraq.Ripoti hiyo ya upande wa Italy inatofautiana na Maelezo yaliyotolewa na Marekani siku ya juamamosi amabapo wanajeshi wa Marekani wameondolewa lawama. Hata hivyo ripoti ya marekani imepingwa vikali na Italy. Mgongano huo wa Ripoti unatishia kuzidisha mgawanyiko kati ya Italy na Marekani kuhusu mauaji hayo.