ROME: Makadinali wajitayarisha kumchagua Papa mpya
17 Aprili 2005Matangazo
Vatikan imetoa maelezo ya utaratibu utakaofuatwa kumchagua kwa siri Baba Mtakatifu mpya.Uchaguzi wa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki utaanza siku ya Jumatatu.Msemaji wa Vatikan amesema ishara za moshi kutoka paa la kanisa dogo la Sistine,kuujulisha ulimwengu ikiwa Papa mpya ameteuliwa au la,zinatarajiwa kuonekana wakati wa mchana na kama saa moja jioni kila siku ya upigaji kura.Walinzi wa usalama katika Vatikan wameimarisha ukaguzi,kuhakikisha kuwa hakuna atakaejipenyeza kuwachungulia makadinali 115 watakaomchagua mrithi wa marehemu Yohana Paulo wa Pili.