1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Makadinali wa Kikatoliki wameingia katika makaazi ya St. Martha kujitayarisha kwa kazi ya kumchagua Pope mpya.

18 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLo

Makadinali wa Kikatoliki wamefanya misa katika kanisa kuu la St. Peter Basilica huko Vatican. Misa hiyo imefanyika kabla ya kikao cha baraza la siri la makadinali ambalo litamchagua kiongozi mwingine wa kanisa hilo baada ya kifo cha Pope John Paul wa pili. Jumla ya makadinali 115 wakataa katika makaazi ya Santa Marta huko Vatican, bila ya mawasiliano na sehemu nyingine za nje, hadi pale watakapofanikiwa kumchagua Pope mpya kuazia baadaye leo.

Watapiga kura mara nne kila siku. Moshi utafuka kutoka katika kanisa dogo la Sistine mara mbili kila siku lakini ni moshi mweupe tu ndio utaashiria kuwa Pope mpya amekwisha patikana.