Rome. Makadinali kukutana katika baraza la siri kumchagua kiongozi mwingine wa kanisa Katoliki.
10 Aprili 2005Matangazo
Kanisa Katoliki limeanza siku tisa rasmi za maombolezo kutokana na kifo cha kiongozi wa kanisa hilo Pope John Paul wa pili. Mazishi yalifanyika siku ya Ijumaa katika eneo la St. Peters Basilica mjini Rome.Zaidi ya viongozi 200 wa kisiasa na kidini pamoja na mamia kwa maelfu ya mahujaji walihudhuria mazishi hayo. Misa ya wafu iliyochukua saa tatu iliongozwa na kadinali wa Kijerumani Joseph Ratzinger. Kundi la makadinali linakutana katika baraza la siri kumchagua kiongozi mwingine baada ya marehemu papa Paulo wa pili kuanzia Aprili 18. Hadi pale kiongozi mwingine atakapotajwa, makadinali wameapa kutozungumza na vyombo vya habari.