1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Köhler na Papa wadai hatua zaidi kupiga vita njaa

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7F9

Papa Benedikt wa 13 na Rais Horst Köhler wa Ujerumani wamewataka viongozi duniani kuchukuwa hatua za kuwajibika zaidi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani hapo jana.

Katika makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa mjini Rome Italia Köhler amesema njaa kimsingi inaweza kuwa inatokana na kushindwa kwa hatua za kisiasa. Amesema walaji katika nchi zenye maendeleo ya viwanda duniani wanaweza kuchangia katika kupiga vita njaa kwa kununuwa bidhaa zinazotokana na biashara inayozingatia haki duniani.

Papa Benedikt amesema katika taarifa kwamba utokomezaji wa njaa ni mojawapo ya changamoto kubwa kabisa zinazokabili dunia hivi sasa.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO linakadiria kwamba takriban watu milioni 800 duniani kote wanateseka kutokana na njaa.