1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME Kura ya maoni kuhusu sheria za uzazi yafanyika nchini Itali

13 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF48

Raia wa Itali wanapiga kura ya maoni kuamua ikiwa wanataka kuzilegeza kamba sheria za uzazi wa kusaidiwa. Wapigaji kura wanaulizwa kuamua ikiwa wanataka kufutilia mbali marufuku ya wanawake kutoa mayai yao au wanaume kutoa mbegu zao. Wataamua pia ikiwa wanataka mume na mke wapimwe kujua ikiwa wanaugua magonjwa ya ukoo na ikiwa wanataka utafiti wa viinitete uendelee.

Kiongozi wa kanisa katoliki, papa Benedict wa 16, amewatolea wito wapigaji kura waigomee kura hiyo kwa misingi ya maadili. Asilimia 50 ya wapigaji kura wanatakiwa kushiriki katika kura hiyo ili matokeo yake yakubalike na kuidhinishwa. Wanasiasa kadhaa nchini Itali wameyakosoa makao makuu ya kanisa katoliki, Vatican, kwa kuliingilia kati swala hilo la kisiasa.