ROME: Kura ya maoni juu ya nguvu za uzazi kwa njia za kisayansi yakosa umaarufu
14 Juni 2005Matangazo
Kura ya maoni juu ya kutiwa nguvu uzazi kwa njia ya kisayansi imekosa umaarufu nchini Italy baada ya kuapata chini ya asilimia 50 ambayo ikihitajika kuhalisha zoezi hilo.
Wizara ya mambo ya ndani ya Italy imesema kuwa asilimia 25 pekee ya wapiga kura ndio walioshiriki katika zoezi lililo chukua siku mbili.
Hili ni jaribio la tano la kushindwa kufanikiwa katika kura ya maoni kuhusu mpango wa uzazi kwa njia ya kisayansi nchini Italy ambapo wadadisi wanahisi kuwa watu wengi hawakushiriki kwa sabau ya uoga.
Kanisa katoliki lilitoa wito kwa watu kususia zoezi hilo kwani ni kinyume cha maumbile ya mwanadamu.