1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Italy kutoa ripoti yake juu ya kifo cha Calipari.

2 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFHX

Italia inakusudia kutoa matokeo ya uchunguzi juu ya kifo cha askari wake Nicola Calipari aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na majeshi ya Marekani katika kizuizi cha barabarani mjini Baghdad miezi miwili iliyopita wakati alipokuwa akimsindikiza uwanja wa ndege mwana habari aliyeachiliwa huru baada ya kutekwa nyara.

Marekani ilitoa ripoti yake siku ya jumamosi na ambayo ilisema haitawachukulia hatua za kinidhamu wanajeshi wake waliohusika na kitendo hicho.

Hatua ambayo imezua utata baina ya Washington na mshirika wake wa karibu nchini Iraq.